Lori ya LPG iliyokuwa ikisafirisha mitungi ya gesi yalipuka na kuteketea kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mai Mahiu karibu na Limuru nchini Kenya.

Magari kadhaa yameripotiwa kuteketea kwa moto baada ya mitungi ya gesi iliyokuwa ikisafirishwa kwa lori hilo kulipuka eneo la Mutarakwa kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru.
Idadi ya waliojeruhiwa au kufariki haijafahamika kufikia sasa.