Waziri Wa Elimu prof. George Magoha asqonya walimu dhidi ya kuwachapa wanafunzi kwa viboko na kuwakumbusha kuwa bado ni hatia katika shule nchini Kenya.
Waziri Magoha amesema kuwa Mwalimu atakaebainika akimchapa au kuwachapa wanafunzi atachukuliwa hatua kulingana na Sheria za kenya.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya mwanafunzi wa umri wa miaka 13 kuadhibiwa shuleni na kujeruhiwa vibaya na walimu wake kwa kutumia bomba la kuchota maji kwa sababu ya kula chapati tano badala ya ile aliyopewa na shule.
Walimu wameshutumiwa kwa kumpiga mvulana huyo kwa kutumia bomba la kuchota maji lakini uongozi wa shule unasema ni wanafunzi wenzake waliofanyia hivyo.
Madaktari katika hospitali hiyo walisema mvulana huyo aliumizwa figo vibaya na sehemu zake za siri pia zilijeruhiwa.
Hata hivyo, shule hiyo iliyoko eneo la Mombasa nchini Kenya imefungwa Na Maafisa wa Elimu wa eneo hilo kwa kutokidhi masharti ya usajili na Usagi wa wizara hiyo baada ya kukaguluwa kufuatia tukio hilo.
Absolutely correct