Mwalimu afikishwa mahakamani kwa chapisho la uongo kwenye Facebook

Mwalimu wa kiume mwenye umri wa miaka 31 ambaye aliandika ujumbe potofu kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akidai kuwa bosi wa TSC Nancy Macharia amefariki alikamatwa na DCI wikendi hii na  amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji mitandaoni na kuchapisha taarifa za uongo.

Jeremiah Mwavuganga Samuel, mwalimu wa Shule ya Msingi ya Musiini iliyoko katika kaunti Makueni nchini Kenya amefikishwa mbele ya mahakama ya Milimani alikana mashtaka hayo mawili ambayo inadaiwa kuwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 16 na 20 mwaka huu, kwa pamoja na wengine ambao hawakufika mahakamani, kwa kutumia akaunti yake ya Facebook aliandika madai ya uongo dhidi ya Macharia ambayo yanadaiwa kulenga kumtia hofu.

Aliandika

Kwa mujibu wa DCI, Mwalimu huyo alikamatwa Jumamosi hii katika Kituo cha Ununuzi cha Makutano huko Nzaui, Makueni baada ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kufanya uchunguzi wa kina wa kitaalamu ili kubaini mtuhumiwa.

Operesheni hiyo iliendeshwa na DCI Emali na wapelelezi wa Taasisi ya Utafiti wa Uhalifu na Ujasusi.

Hata hivyo mwalimu huyo, ambaye amefundisha shuleni hapo kwa miaka minne, alipatikana akiwa na simu iliyotumiwa kuunda chapisho hilo la uongo kuhusu kifo cha Macharia.

Wakati huo huo, DCI imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii dhidi ya kueneza habari potofu, na kutishia hatua dhidi ya wahusika.

Kesi hiyo itatajwa Februari 8.

Leave a Reply