Mashabiki wafariki katika mechi ya AFCON Cameroon

Watu sita wameripotiwa kufariki na  kadhaa kujeruhiwa katika msongamano mkubwa wa watu uliotokea nje ya uwanja unachezewa mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la AP,Rais wa Cameroon Naseri Paul Biya, amesema kuwa huenda kukawa na idadi zaidi ya waathiriwa wa msongamano huo katika lango la uwanja wa Olembe uliopo katika mji mkuu Yaounde.

Watu wapatao 50,000 walikuwa wakijaribu kuingia ndani ya uwanja huo ambao una uwezo wa kuwapokea watu 60,000, lakini kwasababu ya masharti ya kuzuia maambukizi ya Covid 19 ulipaswa kupokea 80% pekee ya watu hao. Hivyo kusababisha mkanyagano ambao pia ulipelekea watoto kadhaa kupoteza fahamu.

Picha ya Mashabiki wakiwasaidia waathiriwa nje ya lango la uwanja wa Olembe.

Muuguzi Olinga Prudence aliliambia shirika la habari la AP kwamba baadhi ya majeruhi walikuwa katika “hali mbaya”.

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limesema katika taarifa yake kwamba kwa sasa “linachunguza hali na kujaribu kupata taarifa zaidi za kile kilichotokea”.

Cameroon ni mwenyeji wa Kombe la Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 50. Taifa hilo la Afrika ya Kati lilikusudiwa kuandaa mashindano hayo mwaka wa 2019 lakini mashindano hayo yaliondolewa mwaka huo na kupewa Misri kwa sababu ya wasiwasi mkubwa kuhusu maandalizi ya Cameroon, hasa utayari wa viwanja vyake.

Uwanja wa Olembe ulikuwa ni miongoni mwa viwanja vilivyokuwa chini ya uangalizi. Ndio uwanja mkuu wa mashindano ya mwezi mzima na utaandaa michezo mingine mitatu, ikijumuisha fainali mnamo Februari 6.Tukio la Jumatatu lilikuwa pigo kubwa la pili kwa nchi katika muda wa siku moja, baada ya watu wasiopungua 17 kufariki wakati moto ulipoanzisha mfululizo wa milipuko katika klabu ya usiku huko Yaounde siku ya Jumapili.

Kufuatia tukio hilo, Rais wa Cameroon Paul Biya aliitaka nchi hiyo kuwa macho wakati ikiandaa hafla yake kubwa ya kitaifa ya michezo katika nusu karne.

Mechi hiyo ya 16 baina ya Cameroon na Comoro, ilichezwa licha ya tukio hilo na ilimalizika kwa ushindi wa wenyeji Cameroon wa 2-1 dhidi ya Comoro na kutinga robo fainali.

Leave a Reply