Waziri mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo anaendelea na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.
Taarifa kutoka kwa mtoto wa mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa, zinasema kuwa kiongozi huyo amelazwa katika hospitali hiyo kwa karibu wiki nzima baada ya kupatwa na matatizo ya tumbo na kufanyiwa upasuaji.
“Baba alilazwa Muhimbili kama siku tano zilizopita. Alifanyiwa upasuaji wa tumbo, lakini bahati mbaya alipatwa na changamoto kidogo,” amesema Fredrick.
Fredrick amewaomba watanzania kuendelea kumuombea ili afya yake iendelee kuimarika.